Ratiba ya Mtihani wa Kidato Cha Pili 2024 | Ratiba ya Mtihani wa NECTA Form Two
Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA) limetoa rasmi ratiba ya mtihani wa Kidato cha Pili kwa mwaka 2024, maarufu kama Form Two National Assessment (FTNA). Mtihani huu unafanyika kwa lengo la kutathmini uwezo wa wanafunzi na maarifa waliyojipatia ndani ya miaka miwili ya mwanzo ya masomo ya sekondari ya kawaida. Ratiba hii inaonyesha mpangilio wa kina wa mitihani ikiwa na tarehe, nyakati, na masomo, ambayo itawasaidia wanafunzi, walimu na wazazi kupanga na kujiandaa vyema kwa mitihani hii muhimu.
Mtihani wa Kidato cha Pili wa NECTA unawaandaa wanafunzi kwa masomo yao ya kidato cha tatu na na cha nne. Kufanya vizuri katika mitihani hii kunawawezesha wanafunzi kujenga msingi imara wa taaluma zao, jambo ambalo litawasaidia kwenye nmtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari. Kwa hivyo, kuwa na ratiba sahihi ya mitihani ni jambo la msingi kwa wanafunzi, walimu, na wazazi.
Ratiba ya Mtihani wa Kidato Cha Pili 2024: Tarehe na Muda Muhimu
Mtihani wa NECTA kwa Kidato cha Pili (FTNA) utaanza rasmi Jumatatu, tarehe 28 Oktoba 2024, na kumalizika Alhamisi, tarehe 7 Novemba 2024. Katika kipindi hiki, wanafunzi watafanya masomo mbalimbali kama vile Uraia, Kiswahili, Hisabati, Biolojia, Kiingereza, Jiografia, Kemia, Historia, Kilimo, Uhasibu, Biashara na mengine mengi.
Kila mtihani utapangwa kufanyika asubuhi au mchana, ili kutoa nafasi ya kupanga vizuri mchakato mzima wa mitihani.
Hii Apa Picha ya Ratiba ya Mtihani wa Kidato Cha Pili 2024
Kama unahitaji kupakua ratiba kamili katika mfumo wa PDF basi unaweza ipata rasmi katika tovuti ya NECTA pamoja na taarifa za mitihani yote inayotarajiwa kufanyika katika kipindi cha mtihani huu. Kwa kuwa na ratiba hii, wanafunzi na walimu wanaweza kupanga vizuri vipindi vya marudio na kujiandaa kwa masomo muhimu. Bofya Hapa Kupakua PDF ya ratiba ya mtihani wa kidato cha pili
Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Katika Mtihani wa Kidato Cha Pili 2024
NECTA imeweka kanuni na miongozo maalum ambayo wanafunzi wanapaswa kufuata wakati wa mitihani. Kanuni hizi zinalenga kuhakikisha kuwa mtihani unafanyika kwa uadilifu na nidhamu kubwa. Zifuatazo ni baadhi ya maelekezo muhimu kwa wanafunzi:
- Wanafunzi wanatakiwa kufanya mtihani kwenye kituo walichosajiliwa. Hairuhusiwi kubadilisha kituo bila idhini ya maandishi kutoka NECTA.
- Ni muhimu kwa wanafunzi kufuata maelekezo yote yanayotolewa na msimamizi wa mtihani, wasimamizi wa chumba, au maafisa wa NECTA wakati wa mtihani.
- Wanafunzi wanatakiwa kufika kwa wakati kulingana na ratiba ya mtihani. Mwanafunzi atakayechelewa zaidi ya nusu saa hataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani.
- Ni muhimu kuingia kwenye chumba cha mtihani na vifaa vilivyoidhinishwa tu na NECTA. Vifaa visivyoruhusiwa vitachukuliwa, na hatua kali za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa ikiwa mwanafunzi atajaribu kudanganya au kutumia vifaa visivyoruhusiwa.
- Mawasiliano kati ya wanafunzi wakati wa mtihani hayaruhusiwi. Mwanafunzi anayehitaji msaada anapaswa kuinua mkono na kuwaita wasimamizi wa chumba.
- Wanafunzi wanatakiwa kuandika namba zao za mtihani kwa usahihi kwenye kila ukurasa wa kijitabu cha majibu. Kuandika jina, majina ya utani, au alama za kipekee ni ukiukaji wa kanuni za mtihani na kunaweza kusababisha kufutwa kwa matokeo.
- Udanganyifu wowote unaogundulika unaweza kusababisha mwanafunzi kutolewa nje ya mtihani na kufutiwa matokeo yote.
- Kila maandiko katika mtihani yanapaswa kuandikwa kwa wino wa bluu au mweusi, na michoro yote inapaswa kufanywa kwa penseli.
Weka maoni yako