Mechi ya Yanga Leo Dhidi ya Tabora United 02/04/2025 NBC: Yanga SC yataka kulipa kisasi dhidi ya Tabora United Ni mechi ya marudiano! Ndivyo tunavyoweza kuielezea mechi ya Yanga SC dhidi ya Tabora United itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanashuka dimbani wakiwa na lengo kuu moja: kulipiza kisasi na kupata pointi tatu muhimu katika harakati zao za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League).
Mechi ya Yanga Leo Dhidi ya Tabora United 02/04/2025 NBC
Kumbukumbu ya kichapo katika raundi ya kwanza Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 7, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Tabora United iliwashangaza wengi kwa kuifunga Yanga SC mabao 3-1. Matokeo haya yalikuwa ni miongoni mwa machache yaliyoitikisa Yanga msimu huu, na sasa timu hiyo inataka kumaliza deni hilo kwa ushindi mnono.
Kauli ya Wachezaji wa Yanga SC Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto amedhihirisha dhamira ya timu hiyo kwa kusisitiza kuwa wapo tayari kupata ushindi na kulipa kisasi kwa wapinzani wao.

“Wametuumiza sana kwa kufunga mabao matatu, tupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa, nawaambia Tabora United kwa niaba ya wachezaji wenzangu walikuja kwa ajili yetu, lakini sasa tupo kwao, tunataka pointi tatu, tumejipanga vyema kwa ajili ya kurejea,” Mwamnyeto alisema.
Mtazamo wa Kocha Miloud Hamdi Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi anatarajia mechi ngumu kutokana na rekodi ya Tabora United, lakini amesisitiza kikosi chake kipo tayari kuonyesha ubora wao/Mechi ya Yanga Leo Dhidi ya Tabora United 02/04/2025 NBC.
“Mechi hii haitakuwa rahisi kwa sababu tunacheza dhidi ya timu iliyotushinda katika mzunguko wa kwanza, lakini tuko tayari kuonyesha kuwa sisi ni timu kubwa,” Hamdi alisema.
Umuhimu wa mechi hii kwa Yanga SC Kwa Yanga SC, ushindi katika mechi hii ni muhimu si tu kwa kulipiza kisasi, bali pia kuimarisha zaidi uongozi wao kwenye msimamo wa ligi. Mabingwa hao wanahitaji pointi tatu ili kukaa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao na kujiandaa vyema na mechi zijazo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako