Nafasi za Kazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2025 Zanzibar: Mratibu wa Uchaguzi (Unguja na Pemba). Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza nafasi zilizoachwa wazi Zanzibar kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi maalum za usimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025 Tanzania, Zanzibar (Unguja, na Pemba).
Nafasi hizo zinalingana na nafasi ya Mratibu wa Uchaguzi, ambapo nafasi moja ipo Unguja na nyingine Pemba.
Nafasi za Kazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2025 Zanzibar
Majukumu ya Mratibu wa Uchaguzi
Kuratibu habari na taarifa zote zinazohusiana na uchaguzi.
Kuratibu upatikanaji wa vifaa na nyenzo muhimu zitakazotumika kufanikisha uchaguzi.
Kuwa kiunganishi kati ya Tume ya Uchaguzi, watendaji wa uchaguzi wa wilaya/majimbo na wadau wengine.
Kushirikiana na kushauriana na wasimamizi wa uchaguzi katika eneo lake.
Sifa za Mwombaji wa Nafasi ya Mratibu wa Uchaguzi

Mwombaji anayehitaji kuchukua nafasi hii ni sharti awe na sifa zifuatazo:
Awe raia wa Tanzania.
Awe Mtumishi wa Umma.
Awe na Shahada au Stashahada ya Juu kutoka katika fani yoyote.
Awe mwadilifu na mkweli.
Awe mkazi wa eneo analoomba (Pemba au Unguja).
Awe tayari kujituma na kufanya kazi hata pasipo kusimamiwa kwa karibu.
Awe na uzoefu katika masuala ya Uchaguzi, Uandikishaji wa Wapiga Kura, au Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Awe hajawahi kuhukumiwa au kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai au kufungwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
Waombaji wanashauriwa kuzingatia kwa makini vigezo vyote vilivyowekwa na Tume kabla ya kutuma maombi yao. Kushindwa kukidhi mahitaji yoyote hapo juu kutasababisha kukataliwa kwa maombi/Nafasi za Kazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2025 Zanzibar.
Kwa waombaji wote wanaotaka kuomba nafasi hizo muhimu za kitaifa, ni vyema wakachukua hatua mapema, kuandaa nyaraka zinazohitajika, na kuhakikisha wanafuata maelekezo yote yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako