Kikosi cha Simba Leo vs Al Masry 09/04/2025, Simba dhidi ya Al Masry kwenye kombe la shirikisho la CAF. Klabu ya Simba SC ya Tanzania maarufu kwa jina la Mnyama itacheza kwa mara ya kwanza leo Jumatano Aprili 9, 2025 dhidi ya Al Masry ya Misri katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huu muhimu utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 Jioni (Saa za Afrika Mashariki). Simba imetangaza rasmi kuwa timu iko tayari na ina matumaini makubwa ya kusonga mbele. “Hii Tunavuka!” Kauli hii inaonyesha kujiamini na ari ya hali ya juu kabla ya awamu ya mchujo.
Mashabiki wa Simba SC wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao kwenye uwanja wao wa nyumbani. Ushindi katika mechi hii utaihakikishia Simba kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025, hatua ya kihistoria kwa klabu hiyo.
Kikosi cha Simba Leo vs Al Masry 09/04/2025
Kikosi kinachoaza leo
- CAMARA
- KAPOMBE
- CHAMOU
- M. HUSSEIN ©
- HAMZA
- NGOMA
- KAGOMA
- AHOUA
- MPANZU
- KIBU
- MUKWALA

Mashabiki wa soka barani Afrika pia wanatarajia mechi yenye ushindani mkubwa, hasa kutokana na ubora wa timu zote mbili. Mashabiki wanaohudhuria uwanjani hapo wanakumbushwa kufuata taratibu za usalama na kufika mapema ili kuepusha msongamano wa watu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako