Fadlu David Kuwajibika Iwapo Simba Itaondolewa na Al Masry: Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema yuko tayari kuwajibika kwa matokeo yoyote mabaya endapo timu yake itashindwa kufuzu hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu David Kuwajibika Iwapo Simba Itaondolewa na Al Masry
Akizungumza kabla ya mechi ya mkondo wa pili dhidi ya Al Masry ya Misri, Davids alisema:
“Nipo hapa Simba kwa ajili ya mafanikio na siyo kuona timu kubwa kama hii inafeli. Hahaha! Wachezaji wangu nimewaruhusu wacheze kwa staili fulani na kama wanapoteza au wanashindwa kufikia malengo ni mimi ndiye ninayewajibika…! Ni mara zote inakuwa hivyo.”
Mchezo huu muhimu utapigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 Jioni. Simba inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kwa kauli hii, Davids anaonyesha uwajibikaji mkubwa na dhamira ya kweli katika kusaka mafanikio kwa klabu hiyo kubwa ya Tanzania. Watazamaji na mashabiki wanatarajia kuona matokeo chanya kutoka kwa wawakilishi wa Tanzania.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako