Ratiba Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB 2024/2025 | SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa Kombe la Shirikisho Benki ya CRDB, wametangaza ratiba rasmi ya mechi za robo fainali msimu wa 2024/2025.
Mechi hizi zinasubiriwa kwa hamu na mashabiki kote nchini hasa kutokana na ushiriki wa klabu kubwa za Simba SC na Yanga SC.
Mechi zote zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD na Azam Sports 2 HD, hivyo mashabiki wanaweza kufuatilia matukio yote muhimu bila kukosa.
Mashabiki wanashauriwa kufuata ratiba rasmi na kutazama mechi kupitia vyombo vya habari vilivyoidhinishwa ili kuepuka taarifa potofu. Inashauriwa pia kuzuia ununuzi wa tikiti kwa njia zisizo halali.
Ratiba Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB 2024/2025
Jumapili, Aprili 13 | Saa 10:00 Jioni
Simba SC vs Mbeya City
Jumatatu, Aprili 14 | Saa 10:00 Jioni
JKT Tanzania vs Pamba Jiji
Singida B.S vs Kagera Sugar
Jumanne, Aprili 15 | Saa 10:00 Jioni
Yanga SC vs Stand United

Robo fainali hizi zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikiwania kutinga nusu fainali. Mashabiki wa soka nchini wanatarajiwa kushuhudia vipaji, mbinu, na ushindani wa hali ya juu wa vilabu kadhaa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako