Matokeo ya Yanga Leo vs Stand United 15/04/2025 | Yanga SC itamenyana na Stand United Jumanne hii katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.
Michuano ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB inatarajiwa kuhitimishwa rasmi Jumanne hii kwa mchezo mkali kati ya Yanga SC na Stand United FC.
Mechi hiyo itaanza saa 10:00 Jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Wananchi itaendeleza ubabe wake au Stand United itawashangaza wengi kwa kuwanyima Yanga ubingwa na kutinga hatua ya nusu fainali.
Mchezo huu wa mwisho wa robo fainali utakuwa na mvuto wa kipekee, ukizingatia historia ya Yanga SC katika michuano hii na kiu ya Stand United kuweka historia ya kutinga nusu fainali. Kwa mashabiki ambao hawatakuwepo uwanjani, kuna fursa ya kutazama mechi hii moja kwa moja kupitia AzamSports1HD.
Matokeo ya Yanga Leo vs Stand United 15/04/2025
FT | YANGA 8:1 STAND UNITED
- FT: Yanga SC 8-1 Stand United
- 86′ Kennedy Musonda anaingia kwenye kitabu cha wafungaji naye leo
- 63′ Aziz tena anaweka la saba
- 60′ Azizi Ki anaweka hattrick kwa goli la 6 kwa Yanga
- 51′ Aziz Ki anaweka chuma ya 5 na goli la pili kwake kwa free kick
- HT: Yanga SC 4-0 Stand United
- 41′ Chama anaweka goli la 4 na lapili kwake kwenye mchezo
- 32′ Chama anafunga goli la 3 la mchezo
- 20′ Kibabage anafunga goli la kutanua mchezo
- 16′ Aziz Ki anafungua kurasa ya magoli kwa Yanga
- mchezo kuaaza saa 10:00

Mpaka sasa, timu tatu tayari zimefuzu hatua ya nusu fainali, nazo ni:
Simba SC
Singida Big Stars
JKT Tanzania
CHECK ALSO:
Weka maoni yako