Viwanja na Tarehe ya Nusu Fainali Kombe la CRDB Federation Cup 2024/2025

Viwanja na Tarehe ya Nusu Fainali Kombe la CRDB Federation Cup 2024/2025: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viwanja na tarehe rasmi za mechi za nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB kwa msimu wa 2024/2025. Nusu fainali hizi zimepangwa kufanyika kati ya Mei 16 na 18, 2025.

Mashindano haya ni sehemu ya kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya udhamini wa Benki ya CRDB. Timu nne zilizofuzu kwa nusu fainali zimeonyesha uwezo mkubwa katika hatua za awali, na mashabiki wanatarajia mechi zenye ushindani mkubwa.

Viwanja na Tarehe ya Nusu Fainali Kombe la CRDB Federation Cup 2024/2025

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, timu zinazowania tiketi ya fainali zitakutana kama ifuatavyo:

Viwanja na Tarehe ya Nusu Fainali Kombe la CRDB Federation Cup 2024/2025
Viwanja na Tarehe ya Nusu Fainali Kombe la CRDB Federation Cup 2024/2025
  1. Young Africans vs JKT Tanzania
    Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

  2. Simba SC vs Singida BS
    Mchezo huu utafanyika katika Uwanja wa Tanzanite, Kwarara mkoani Manyara.

Mashabiki wanaombwa kufuata ratiba rasmi na kufika viwanjani kwa wakati. Pia wanatakiwa kuzingatia kanuni za usalama na maelekezo kutoka kwa waandaaji wa mashindano. Tikiti zinatarajiwa kuuzwa kwa njia ya kielektroniki, hivyo ni muhimu kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu.

Nusu fainali hizi ni hatua muhimu kuelekea kumpata bingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024/2025. Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kupata burudani ya kipekee kutoka kwa vigogo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

CHECK ALSO: