Thamani ya Mkataba wa Simba na Jayrutty Kutengeneza Jezi: Simba SC Yasaini Mkataba wa Bilioni 38 na JAYRUTTY kwa Jezi, Uwanja na Maboresho ya Miundombinu.
Thamani ya Mkataba wa Simba na Jayrutty Kutengeneza Jezi
Klabu ya Simba Sports Club imeingia katika hatua mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya JAYRUTTY Investment Company Limited wenye thamani ya shilingi bilioni 38. Kupitia mkataba huu, JAYRUTTY ilipewa zabuni rasmi ya kutengeneza na kusambaza jezi na vifaa vyote vyenye nembo ya Simba SC.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, JAYRUTTY Investment pia imetia saini makubaliano ya kimataifa na Diadora, kampuni inayoongoza duniani ya vifaa vya michezo. Kupitia ushirikiano huu, Diadora itahusika moja kwa moja na utengenezaji wa jezi na vifaa vyote rasmi vya Simba Sports Club, hivyo kuiweka Simba kwenye ramani ya vilabu vinavyovaa chapa za kimataifa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Mbali na utengenezaji wa jezi na vifaa, mkataba huu pia unajumuisha maboresho makubwa ya miundombinu ya klabu. Kampuni ya JAYRUTTY Investment imeahidi kujenga uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki kati ya 10,000 na 12,000 katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam. Uwanja huu unatarajiwa kuwa sehemu ya kimkakati ya maendeleo ya Simba na kutoa mazingira bora ya mazoezi na mechi kwa klabu.
Katika hatua nyingine ya kuboresha huduma na utawala wa klabu, Jayrutty pia atapata basi jipya la Irizar kwa ajili ya timu hiyo na kujenga ofisi mpya ambazo zitakuwa makao makuu ya klabu hiyo barani Afrika.
Mkataba huu wa kimkakati unaonyesha dhamira ya Simba katika kuongeza ubora ndani na nje ya uwanja. Mashabiki wanatarajiwa kunufaika na bidhaa bora, miundombinu ya kisasa, na maendeleo ya kiutawala yatakayoiweka Simba katika kiwango cha juu cha ushindani kitaifa na kimataifa/Thamani ya Mkataba wa Simba na Jayrutty Kutengeneza Jezi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako