Jayrutty Kusajili Mchezaji Mmoja Simba Kila Mwaka

Jayrutty Kusajili Mchezaji Mmoja Simba Kila Mwaka | Katika kuendeleza ushirikiano wa kipekee kati ya Kampuni ya JAYRUTTY Investment na Simba Sports Club, mwanzilishi na rais wa kampuni hiyo CPA Joseph Rwegasira ametangaza mpango mpya wa kuwashirikisha moja kwa moja mashabiki wa Simba katika usajili wa wachezaji.

Jayrutty Kusajili Mchezaji Mmoja Simba Kila Mwaka

Akizungumza katika hafla hiyo ya kutangaza makubaliano ya kimkakati kati ya pande hizo mbili, CPA Rwegasira alieleza kuwa kila mwaka JAYRUTTY Investment itasimamia na kugharamia usajili wa mchezaji anayependekezwa na mashabiki wa Simba.

Alisema, “Kila mwaka tutasajili mchezaji mmoja ambaye Wanasimba wanamtaka, tutakuwa tunaambiwa na sisi tutakuwa tunamsajili.”

Hatua hii inalenga kuongeza ushiriki wa mashabiki katika maamuzi ya kimkakati ya klabu na kuwaruhusu kuchangia moja kwa moja katika maendeleo ya kikosi cha timu yao pendwa.

Jayrutty Kusajili Mchezaji Mmoja Simba Kila Mwaka
Jayrutty Kusajili Mchezaji Mmoja Simba Kila Mwaka

Mpango huu unakwenda sambamba na mikakati mingine muhimu inayotekelezwa na kampuni ya JAYRUTTY Investment kwa klabu ya Simba SC, ikiwa ni pamoja na mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 38, uzalishaji na usambazaji wa jezi za kimataifa kupitia chapa ya Diadora, ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Bunju, ununuzi wa basi jipya la Irizar, na ujenzi wa makao makuu ya klabu mpya.

Mpango huu mpya wa kuwashirikisha mashabiki katika usajili unawakilisha dhamira ya kweli ya JAYRUTTY ya kuwekeza katika maendeleo ya Simba SC, si tu katika masuala ya miundombinu bali pia katika kuongeza ari na ushirikiano kati ya mashabiki na uongozi wa klabu hiyo.

CHECK ALSO: