Ahadi 10 za Mzabuni Mpya wa Jezi za Simba Jayrutty Investment Company Limited | Ujenzi wa Viwanja, Kituo cha Matibabu na Motisha kwa Mashabiki.
Ahadi 10 Muhimu kutoka kwa Mzabuni wa New Jersey wa Simba SC – Jayrutty Investment Co. Ltd/Ahadi 10 za Mzabuni Mpya wa Jezi za Simba Jayrutty Investment Company Limited.
Klabu ya Simba Sports Club imekaribisha ujio wa mzabuni mpya wa jezi zake aina ya Jayrutty Investment Co. Limited ambayo imeweka dira ya maendeleo yenye ahadi 10 zinazolenga kuimarisha miundombinu, ustawi wa timu na kuchangia mashabiki.
Ahadi hizi zinaonyesha dhamira ya kweli ya kubadilisha taswira ya klabu na kuiwezesha Simba kuwa taasisi ya kisasa na yenye ushindani mkubwa barani Afrika/Ahadi 10 za Mzabuni Mpya wa Jezi za Simba Jayrutty Investment Company Limited.
Ahadi 10 za Mzabuni Mpya wa Jezi za Simba Jayrutty Investment Company Limited
Hizi ndizo ahadi 10 za mzabuni mpya:

Ukarabati wa Viwanja vya Mazoezi:
Viwanja vya mazoezi vya klabu vitafanyiwa maboresho makubwa ili kuwapa wachezaji mazingira bora ya kujiandaa kwa mashindano mbalimbali.Ujenzi wa Uwanja wa Mechi:
Kujengwa kwa uwanja wa kisasa utakaoweza kuhudumia mashabiki kati ya elfu 10 hadi elfu 12, hatua itakayoongeza mapato na kuimarisha mahusiano ya timu na mashabiki.Basi la Kisasa kwa Timu Kubwa:
Timu itapatiwa basi la kisasa lenye hadhi ya klabu kubwa, linalotoa huduma bora kwa wachezaji na benchi la ufundi.Kituo cha Matibabu (Medical Center):
Ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa kwa ajili ya huduma za matibabu, uangalizi wa afya za wachezaji, na kuimarisha utimamu wa miili yao kabla na baada ya mechi.Ofisi Mpya za Klabu:
Simba itakuwa na ofisi mpya, zenye mazingira rafiki na ya kisasa kwa uendeshaji wa shughuli za kila siku za klabu.Studio za Habari za Kisasa:
Kitengo cha habari cha Simba kitapatiwa studio za kisasa, zitakazowezesha uzalishaji bora wa maudhui ya habari, vipindi na matangazo kwa mashabiki.Tsh Milioni 100 Kila Pre Season:
Kila kipindi cha maandalizi ya msimu mpya, klabu itapata motisha ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya maandalizi na maandalizi ya kambi.Tsh Milioni 100 Kila Simba Day:
Sherehe ya kila mwaka ya Simba Day itapewa msukumo zaidi kwa kupatiwa milioni 100 kila mwaka.Tsh Milioni 100 kwa Programu za Vijana:
Uwekezaji mkubwa utaelekezwa kwenye programu za kukuza vipaji vya vijana ili kuandaa nyota wa baadaye wa Simba SC.Usajili wa Mchezaji Mmoja Kila Mwaka:
Kila mwaka mzabuni huyo atachangia moja kwa moja usajili wa mchezaji mmoja atakayependezwa, ikiwa ni sehemu ya kuongeza ushindani ndani ya kikosi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako