Matokeo EPL Leo, Arsenal na Chelsea Zapata Ushindi, Man United Yapoteza Nyumbani, Katika mechi za leo za Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal na Chelsea walipata ushindi wa kishindo, huku Manchester United wakiambulia kichapo mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
Matokeo EPL Leo, Arsenal na Chelsea Zapata Ushindi, Man United Yapoteza Nyumbani
Fulham 1-2 Chelsea
Chelsea ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham ugenini.
⚽ 20’ Alex Iwobi (Fulham)
⚽ 83’ George (Chelsea)
⚽ 90+3’ Neto (Chelsea)
Chelsea ilionesha uthabiti mkubwa kipindi cha pili kwa kupindua matokeo na kutoka na alama zote tatu katika dakika za mwisho.
Ipswich 0-4 Arsenal
Arsenal iliendeleza ubabe wake kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Ipswich.
⚽ 14’ Leandro Trossard
⚽ 28’ Gabriel Martinelli
⚽ 69’ Leandro Trossard
⚽ 88’ Ethan Nwaneri
The Gunners walitawala mchezo kwa muda wote na kuimarisha nafasi yao katika msimamo wa ligi.
Manchester United 0-1 Wolves
Manchester United wakiwa nyumbani, walipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Wolves.
⚽ 77’ Pablo Sarabia
Kipigo hiki kinazidi kuweka presha kwa kocha wa Manchester United huku timu ikionekana kupoteza mwelekeo hasa nyumbani.
Matokeo haya yameendelea kubadili hali ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo Arsenal na Chelsea zimeonyesha dhamira ya kuwania nafasi za juu, huku Manchester United ikiendelea kusuasua.
Katika hatua hii ya msimu, kila pointi inahesabiwa. Kupoteza pointi nyumbani kunaweza kuathiri nafasi ya timu kumaliza msimu katika nafasi za juu au kushiriki michuano ya Ulaya.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako