Liverpool Karibu Kutwaa Ubingwa wa EPL 2024/25, Baada ya Arsenal Kulazimishwa Sare

Liverpool Karibu Kutwaa Ubingwa wa EPL 2024/25, Baada ya Arsenal Kulazimishwa Sare na Crystal Palace. Liverpool inakaribia ubingwa wa Premier League, Arsenal ikishindwa na Crystal Palace – Matokeo na msimamo

LIGI Kuu ya Uingereza (EPL) inaelekea ukingoni, huku Liverpool ikiwa imesalia hatua moja tu kutawazwa mabingwa wa msimu wa 2024/2025. Hali imekuwa mbaya zaidi baada ya Arsenal kutoka sare ya 2-2 na Crystal Palace kwenye Uwanja wa Emirates.

Liverpool Karibu Kutwaa Ubingwa wa EPL 2024/25, Baada ya Arsenal Kulazimishwa Sare

Matokeo ya Mchezo: Arsenal 2-2 Crystal Palace

  • ⚽ 03’ Jakub Kiwior (Arsenal)
  • ⚽ 27’ Eberechi Eze (Crystal Palace)
  • ⚽ 42’ Leandro Trossard (Arsenal)
  • ⚽ 83’ Jean-Philippe Mateta (Crystal Palace)

Matokeo haya yameizuia Arsenal kupata pointi walizohitaji ili kuendelea kuwasumbua Liverpool kileleni mwa jedwali la ligi. Kwa sasa, Majogoo hao wa Anfield wanahitaji sare tu katika mechi yao inayofuata ili kujihakikishia rasmi ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine tena.

Msimamo wa EPL (Top 5) Baada ya Mechi za Hivi Karibuni:

Liverpool Karibu Kutwaa Ubingwa wa EPL 2024/25, Baada ya Arsenal Kulazimishwa Sare
Liverpool Karibu Kutwaa Ubingwa wa EPL 2024/25, Baada ya Arsenal Kulazimishwa Sare


1️⃣ Liverpool – Mechi 33 | Pointi 79
2️⃣ Arsenal – Mechi 34 | Pointi 67
3️⃣ Manchester City – Mechi 34 | Pointi 61
4️⃣ Nottingham Forest – Mechi 33 | Pointi 60
5️⃣ Newcastle United – Mechi 33 | Pointi 59

Kukiwa na pengo la pointi 12 kati ya Liverpool na Arsenal, na ukizingatia Arsenal imebakiza mechi moja pekee msimu huu, Liverpool inaonekana tayari imejihakikishia ubingwa. Sare katika mechi inayofuata itatosha kufikia malengo yao.

CHECK ALSO: