Simba vs RS Berkane Fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025

Simba vs RS Berkane Fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025 | Simba SC kumenyana na RS Berkane, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limethibitisha ratiba ya mechi za mwisho za Kombe la Shirikisho msimu wa 2024/2025, ambapo Simba SC ya Tanzania itamenyana na RS Berkane ya Morocco katika hatua ya fainali ya michuano ya kimataifa.

Simba SC imefuzu fainali baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika hatua za awali kwa kuwafunga wapinzani wao kwa jumla ya bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC. Kwa upande mwingine, RS Berkane ameonyesha uzoefu mkubwa katika shindano hili, na fainali hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Simba vs RS Berkane Fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025

  • Mchezo wa Mkondo wa Kwanza:
    🗓 Mei 17, 2025
    📍 Morocco
    RS Berkane vs Simba SC

Simba vs RS Berkane Fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
Simba vs RS Berkane Fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  • Mchezo wa Mkondo wa Pili:
    🗓 Mei 25, 2025
    📍 Tanzania
    Simba SC vs RS Berkane

Kwa Simba SC, hii ni nafasi muhimu ya kuandika historia kwa kutwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza, huku RS Berkane ikilenga kuongeza idadi ya mataji katika michuano hii. Mechi zote mbili zinatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka kote barani Afrika.

Safari ya Simba SC ya Kombe la Shirikisho imefikia hatua ya mwisho, na sasa wanakabiliwa na changamoto ya kuwakabili RS Berkane. Mashabiki na wapenzi wa soka barani Afrika wanasubiri kwa hamu kuona nani ataibuka bingwa wa msimu huu.

CHECK ALSO: