Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto 29/04/2025

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto 29/04/2025 | Nusu fainali ya Kombe la Muungano 2025 inapamba moto huko Gombani

Michuano ya Kombe la Muungano 2025 inaingia katika hatua yake muhimu zaidi, huku Zimamoto FC na Yanga SC zikitarajiwa kumenyana katika nusu fainali ya pili, itakayochezwa Aprili 29, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani.

Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwani mshindi atajikatia fainali dhidi ya JKU SC ambao tayari wamefuzu baada ya kuiondoa Azam FC kwa ushindi wa mabao 2-1. Hii inaashiria kuwa pambano la fainali litakuwa kali na litaleta pamoja timu bora kutoka kila upande.

Timu ya Zimamoto FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Coastal Union inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Aprili 25, 2025. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na mchezaji nyota Rashid Salum dakika ya 28, na kutosha kuipeleka Zimamoto hatua inayofuata.

Katika mechi hiyo, licha ya jitihada kubwa za Coastal Union, walishindwa kurudisha bao la kuongoza, hivyo kuhitimisha safari yao ya kuwania Kombe la Muungano 2025. Mashindano haya yamekuwa na ushindani mkubwa, yakishirikisha timu zenye viwango vya juu na ari ya kutwaa ubingwa.

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto 29/04/2025

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto 29/04/2025
Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto 29/04/2025

Kikosi cha Yanga kinachoaza leo hiki hapa:-

  • Mshery
  • Kibwana
  • Nkane
  • Andabwile
  • Mwamnyeto
  • Mkude
  • Chama
  • Azizi KI
  • Mzize
  • Ikanga Lombo
  • Maxi

CHECK ALSO: