Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil

Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil: CBF imemthibitisha Carlo Ancelotti kama kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil, kocha wa kwanza wa kigeni tangu 1925.

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) lilitangaza rasmi uteuzi wa kocha maarufu wa Italia Carlo Ancelotti kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil. Uteuzi huo unamfanya Ancelotti kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa Brazil tangu 1925, na kufungua ukurasa mpya katika historia ya taifa hilo lenye mafanikio makubwa zaidi kisoka duniani.

Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa CBF, Ancelotti ataanza kazi rasmi Mei 26, 2025, siku moja baada ya klabu yake ya sasa, Real Madrid, kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu ya Uhispania kwa mechi dhidi ya Real Sociedad/Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil.

Ancelotti, 65, anatarajiwa kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, huku nafasi yake ikichukuliwa na Xabi Alonso. Msimu huu, Ancelotti ameshuhudia timu yake ikipata misukosuko, ikiwa ni pamoja na kupoteza mechi nne mfululizo dhidi ya mahasimu wao Barcelona,  wakiongozwa na meneja Hansi Flick.

Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil
Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil

Kocha huyo wa Italia ana historia nzuri katika soka la kimataifa, akiwa na rekodi ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara saba: mara tano kama meneja na mara mbili kama mchezaji. Katika maisha yake ya ukocha, Ancelotti amewahi kufundisha baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, vikiwemo AC Milan, Chelsea, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Juventus, Napoli, Everton, na AC Parma.

CBF ilimsifu Ancelotti kama gwiji wa soka na kocha aliyefanikiwa zaidi katika historia ya mchezo huo, ikiweka wazi kuwa uteuzi wake ni mwanzo wa enzi mpya ya matumaini makubwa kwa Brazil katika maandalizi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026/Carlo Ancelotti Ateuliwa Kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil.

“Ancelotti ni gwiji wa mchezo wa soka kama meneja aliyefanikiwa zaidi katika historia ya soka. Atachukua jukumu rasmi baada ya kumalizika kwa msimu wa 2024/25 wa La Liga, kabla ya kampeni ya Brazil ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA mnamo Juni.”

CHECK ALSO: