Yanga vs JKT Tanzania, Nusu Fainali ya Kwanza CRDB Federation Cup | Mashabiki wa soka Tanzania wanatarajia mpambano mkali na wa kusisimua kati ya Yanga SC na JKT Tanzania katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB msimu wa 2024/2025. Mchezo huu utapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Yanga vs JKT Tanzania, Nusu Fainali ya Kwanza CRDB Federation Cup
Mabingwa watetezi wa taji hili Yanga Sports Club wanaingia uwanjani kusaka nafasi ya kufanikiwa kutetea ubingwa wao. Timu ya Yanga imeonyesha kiwango kizuri katika mashindano ya ndani na nje ya nchi na kubeba matumaini ya mashabiki wao kutinga fainali kwa msimu mwingine mfululizo.
Kwa upande mwingine, JKT Tanzania imefikia hatua hii ikiwa na rekodi nzuri ya kushinda dhidi ya timu ngumu. Wachezaji wa Mafande hao wanaingia uwanjani wakiwa na morali ya hali ya juu wakiamini wanaweza kuweka historia kwa kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB kwa mara ya kwanza.

Muda wa Mchezo: Saa 9:30 Alasiri (15:30 EAT)
Tarehe: Jumapili (Mei 2025)
Uwanja: Mkwakwani Stadium, Tanga
Mbashara: Azam Sports 1 HD
Nani atatinga fainali?
Mashabiki wa soka nchini wanajiuliza:
Je, Yanga SC itaendelea kutawala michuano hii na kutinga fainali tena, au JKT Tanzania itaweka historia kwa kuitoa Yanga na kutinga fainali kwa kishindo?
Majibu yote yatapatikana Jumapili hii Mkwakwani.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako