TAMISEMI Yatangaza Nafasi 694 za Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi: Mwisho wa Maombi Mei 30, 2025.
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza nafasi 694 za walimu wa kujitolea katika shule za msingi nchini kote kupitia Mradi wa GPE-TSP (Global Partnership for Education – Teacher Support Program). Nafasi hizi zimekusudiwa kusaidia shule zilizo na uhaba mkubwa wa walimu, kwa mujibu wa Itifaki ya Ugawaji wa Walimu wa Msingi (P-TAP) mchakato wa ugawaji wa walimu.
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali za mitaa, ambapo walimu waliopewa nafasi hizi watajitolea katika shule za mbali zenye mahitaji makubwa.
TAMISEMI Yatangaza Nafasi 694 za Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi
1.0 Walengwa wa Nafasi Hizi
Nafasi hizi zinalenga wahitimu wa vyuo vya ualimu waliopata Astashahada (Certificate) au Stashahada (Diploma) katika Elimu ya Msingi au Elimu ya Awali kati ya mwaka 2015 hadi 2023.
Wahitimu wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa kielektroniki uitwao Online Teachers Application System (OTEAS) kuanzia 16 Mei hadi 30 Mei, 2025, saa 05:59 usiku kupitia tovuti: https://www.tamisemi.go.tz.

2.0 Sifa za Kitaaluma za Waombaji
Waombaji wanatakiwa kuwa na mojawapo ya sifa zifuatazo:
Mwalimu Daraja la III A: Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi.
Mwalimu Daraja la III B: Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali.
Mwalimu Daraja la III B: Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi.
3.0 Masharti kwa Waombaji wa Nafasi
Waombaji wanapaswa:
Kuwa raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 43.
Kuambatisha vyeti vya kuzaliwa, kidato cha nne/sita na ualimu.
Kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea katika shule za pembezoni zenye uhitaji mkubwa.
Wasiwe waajiriwa wa serikali au taasisi nyingine.
Wasiwe waliowahi kufukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu.
Kuwa na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Kuwasilisha nyaraka zote muhimu kwa usahihi.
Waliosoma nje ya nchi waambatishe namba ya ulinganifu wa matokeo kutoka NECTA.
4.0 Taarifa Muhimu
TAMISEMI Yatangaza Nafasi 694 za Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi, Kwa taarifa zaidi na msaada wa kiufundi, waombaji wanaweza kuwasiliana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia simu namba: 026 2160210 au 0735 160210.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako