Jamus Wawakilisha Sudan Kusini CECAFA Kagame Cup 2025 Itakayofanyika Tanzania Julai Mosi. Jamus Sports Club imetwaa taji la Zain Cup la Sudan Kusini 2024/2025 na kujikatia tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2025, itakayofanyika Tanzania kuanzia Julai 1.
Mechi ya fainali ilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Juba na kuzikutanisha timu mbili zenye nguvu: Jamus SC na El Merriekh SC ya Bentiu. Dakika 90 za mchezo hazikutoa mshindi, baada ya timu zote kushindwa kufungana. Hata hivyo, Jamus SC walipata ushindi wa 4-2 kupitia mikwaju ya penalti.
Jamus Wawakilisha Sudan Kusini CECAFA Kagame Cup 2025
Kipa wa Jamus Majak Mawit Maling ndiye alikuwa shujaa wa mechi hiyo baada ya kuokoa penalti mbili muhimu, hatua iliyoiwezesha timu yake kushinda taji hilo kwa mara nyingine dhidi ya mpinzani wao wa jadi.

Kocha wa Jamus SC Jean Claude Loboko aliwapongeza wachezaji wake kwa ari ya ushindani walioionyesha na juhudi kubwa iliyopelekea ushindi huo. “Wachezaji walifanya kazi kwa bidii, walifuata maelekezo na kuleta heshima kwa klabu na taifa,” alisema kocha huyo.
Jamus SC ilitinga fainali kwa kuifunga Koryrom FC mabao 2-0 katika nusu fainali, huku El Merriekh SC Bentiu ikijikatia tiketi ya kucheza fainali kwa ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Aweil United FC.
Mashindano ya Zain Sudan Kusini Cup 2024/2025 yalidhaminiwa na Zain na kushirikisha zaidi ya timu 30 kutoka sehemu mbalimbali za nchi/Jamus Wawakilisha Sudan Kusini CECAFA Kagame Cup 2025.
Kwa mafanikio hayo, Jamus SC sasa inajiandaa kuiwakilisha Sudan Kusini katika michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2025, itakayofanyika nchini Tanzania kuanzia Julai 1, 2025. Mashindano haya yanazikutanisha klabu bingwa kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
CHECK ALSO:
Weka maoni yako