CAF Kuzindua Kombe Jipya la CAF Champions League Mei 22 | SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limethibitisha kuwa uzinduzi rasmi wa Ligi mpya ya Mabingwa wa CAF utafanyika Mei 22, 2025, mjini Pretoria, Afrika Kusini, kuanzia saa 5:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
CAF Kuzindua Kombe Jipya la CAF Champions League Mei 22
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CAF, hafla hiyo itahudhuriwa na makocha na manahodha wa timu mbili zilizofuzu kwa fainali, ambazo ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Pyramids FC ya Misri. Uzinduzi huo utafanyika siku chache kabla ya mechi ya kwanza ya fainali, iliyopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld.
Kombe jipya la Shirikisho la CAF pia lilizinduliwa.

CAF pia imethibitisha kuwa kombe jipya la CAF Confederation Cup litazinduliwa muda mfupi kabla ya mchezo wa fainali utakaopigwa visiwani Zanzibar. Hii ni hatua muhimu katika kuboresha taswira na hadhi ya mashindano mawili ya vilabu yanayoongoza barani Afrika.
Kuzinduliwa kwa mataji hayo mapya ni sehemu ya mikakati ya CAF ya kuboresha ubora na mvuto wa mashindano ya vilabu barani Afrika, pamoja na kutoa taswira mpya ya kisasa ya soka la Afrika katika ngazi ya kimataifa.
CHECK ALSO:







Weka maoni yako