Haya Hapa Majina ya Vijana Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2025: WANAFUNZI WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2025 KUITWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT – MUJIBU WA SHERIA.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa orodha rasmi ya wanafunzi wa kidato cha sita waliomaliza masomo yao mwaka 2025 na kutakiwa kufanyiwa mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa mujibu wa sheria. Vijana hao wamehitimu kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini na sasa wamepangiwa kujiunga na kambi kadhaa za JKT zilizopo maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Haya Hapa Majina ya Vijana Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2025
Kwa mujibu wa taarifa ya JKT, vijana hao wamegawanywa katika makundi yafuatayo:
Bulombora, Rwamkoma, Msange, Kanembwa, Makutopora, Mpwapwa, Ruvu, Nachingwea, Oljoro, Kibiti, na Maramba.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanafunzi waliotajwa kwenye orodha hiyo wanapaswa kuripoti katika kambi walizopangiwa kuanza mafunzo, kuanzia tarehe ambayo itatangazwa rasmi na mamlaka husika. Wanatakiwa kufuatilia kwa karibu taarifa za JKT ili kupata maelekezo sahihi kuhusu tarehe ya kuripoti na mambo muhimu wanayopaswa kuandaa kabla ya kuelekea kambini.
JKT imesisitiza kuwa zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kuwaandaa vijana kimaadili, kimwili na kiakili sambamba na kuwapatia stadi za maisha zitakazowasaidia kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
Mafunzo haya ya kijeshi kwa mujibu wa sheria, hufanyika kila mwaka kwa wahitimu wa darasa la sita ikiwa ni njia ya kuimarisha uzalendo, nidhamu na mshikamano wa kitaifa miongoni mwa vijana wa Kitanzania.
ANGALIA HAPA MAJINA
CHECK ALSO:
Weka maoni yako