Simba na Singida Black Stars Mchezo wa CRDB, Wote Wako Babati

Simba na Singida Black Stars Mchezo wa CRDB, Wote Wako Babati | Klabu ya Simba SC moja ya vigogo wa soka nchini Tanzania imewasili jijini Arusha leo ikitokea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo muhimu wa FA CRBD federation cup dhidi ya Singida Black Stars. Timu hiyo inatarajiwa kuwasili mjini Babati, Manyara, Mei 31, 2025.

Kwa upande mwingine, mpinzani wao, Singida Black Stars, anatarajiwa kuwasili mjini Babati mchana wa leo akitokea jijini Dar es Salaam. Hii inaonyesha maandalizi makini ya timu zote mbili kwa pambano hili lenye ushindani mkubwa.

Simba na Singida Black Stars Mchezo wa CRDB, Wote Wako Babati

  • Simba SC:

    • Leo: Wamewasili Arusha

    • Kesho (Mei 30): Watakwenda Babati, Manyara

  • Singida Black Stars:

    • Leo jioni: Wataingia moja kwa moja Babati, Manyara

Simba na Singida Black Stars Mchezo wa CRDB, Wote Wako Babati
Simba na Singida Black Stars Mchezo wa CRDB, Wote Wako Babati

Mechi hii ni awamu ya mwisho ya msimu wa 2024/2025 na ina umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili. Simba SC inataka kuifuata Yanga fainali, huku Singida Black Stars ikihitaji ushindi ili kutoa uteja na kutafuta kombe lolote msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maandalizi kwa timu zote mbili yanaendelea vizuri, na mashabiki wanasubiri kwa hamu mchezo huo utakaofanyika Babati, Manyara. Mamlaka za soka na vyombo vya usalama vinatarajiwa kuweka mazingira salama kwa mashabiki na timu zote.

CHECK ALSO: