Yanga Bado Msimamo Wao Kutoshiriki Kariakoo Derby Juni 15 | Klabu ya Young African Sports Club (Yanga SC) imeendelea na msimamo wake wa kutoshiriki mechi ya watani wa jadi, maarufu kwa jina la Kariakoo Derby, inayotarajiwa kuchezwa Juni 15, hadi pale mamlaka husika ya soka nchini itakaposhughulikia madai yake.
Kwa upande wa klabu Afisa Uhusiano wa Yanga SC Ally Kamwe alieleza wazi kuwa Yanga ni klabu ya soka na haina shughuli yoyote nje ya soka. Alisisitiza kuwa klabu hiyo hapo awali ilieleza sababu za msingi za kutochezwa kwa mechi hiyo na madai yake yamewasilishwa rasmi kwenye mamlaka husika.
Yanga Bado Msimamo Wao Kutoshiriki Kariakoo Derby Juni 15
“Tuliwasilisha matakwa yetu kutokana na kilichofanya mechi isichezwe. Kama yatakuwa yamefanyiwa kazi, mechi itachezwa. Lakini hadi tunaingia kwenye kikao, msimamo wetu ni ule ule: HATUCHEZI NG’O,” alisema Kamwe.
Alifafanua kuwa wachezaji wa Yanga wapo tayari kwa mechi na wana ari kubwa kutokana na marupurupu wanayopata katika michezo mikubwa kama hii, lakini wanaheshimu uongozi na taasisi ya klabu.
“Wanasema kitakachoamuliwa na viongozi wetu, watakifanya. Hivyo kwa sasa wanasubiri,” aliongeza Kamwe.

MATAKWA RASMI YA YANGA SC ILI KUSHIRIKI DERBY:
-
Katibu Mkuu wa TFF ajiuzulu
-
Kamati ya Usimamizi ya Ligi ivunjwe
-
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Bodi ya Ligi ajiuzulu
-
Bodi ya Ligi iwe chombo huru na kisichokuwa na mgongano wa maslahi
Katika kikao maalum kilichoitishwa kujadili hatma ya mechi hiyo, uongozi wa Yanga SC uliwasilisha msimamo huo mbele ya Bodi ya Ligi, huku baadhi ya viongozi wakuu wa klabu wakihudhuria kikao hicho.
Viongozi wa Yanga SC Waliohudhuria Kikao cha Bodi ya Ligi:
-
✅ Arafat Haji – Makamu wa Rais
-
✅ Andre Mtine – Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)
-
✅ Alex Ngai – Mjumbe
-
✅ Rodgers Gumbo – Mjumbe
-
âś… Advocate Kalage
-
✅ Ally Kamwe – Afisa Habari
Baada ya kikao hicho, uongozi wa Young Africans ulitangaza kuwa haitoleta timu uwanjani tarehe 15 Juni 2025, hadi pale matakwa yao yote yatakapotimizwa kikamilifu/Yanga Bado Msimamo Wao Kutoshiriki Kariakoo Derby Juni 15.
Kwa mara nyingine, sintofahamu kuhusu Kariakoo Derby imezidi kutokota. Hatma ya mcezo huo mkubwa wa soka la Tanzania iko mikononi mwa mamlaka za juu za soka, huku presha ya mashabiki ikiendelea kupanda.Yanga Bado Msimamo Wao Kutoshiriki Kariakoo Derby Juni 15
CHECK ALSO:








Weka maoni yako