Yanga Yatishia Kutoicheza Fainali ya Kombe la CRDB Dhidi ya Singida Black Stars | Chanzo kikisemwa ni Malipo ya Ubingwa wa Msimu Uliopita.
Yanga SC imetangaza kutoshiriki fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars iwapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadhamini wa Kombe hilo watashindwa kutimiza wajibu wao wa kulipa fedha za klabu kutokana na ubingwa wa msimu uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya uongozi wa klabu hiyo, uamuzi huo umetokana na kushindwa kufanya malipo kwa mabingwa hao wa kihistoria wa soka Tanzania. Yanga SC imesisitiza kuwa haitaingia uwanjani kushiriki fainali hadi haki yake ya msingi ya kifedha itakapotimizwa.
Yanga Yatishia Kutoicheza Fainali ya Kombe la CRDB Dhidi ya Singida Black Stars

anga SC imesisitiza kuwa haitaingia uwanjani kushiriki fainali hiyo mpaka haki yao ya msingi ya kifedha itakapotekelezwa.
“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa HATUTACHEZA mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa Mamlaka za Soka kwa muda mrefu sana, sasa imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia HATUCHEZI. Ally Kamwe – Meneja Habari na Mawasiliano.
Hatua ya Yanga SC kutishia kutoshiriki katika fainali ya Kombe la CRDB inaleta changamoto kubwa kwa wadau wa soka, hasa kwa upande wa maandalizi ya fainali hiyo. Vilevile, inaweza kuathiri taswira ya mashindano, uaminifu wa udhamini na motisha kwa klabu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako