Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza

Vigezo vinavyotumika kuchagua wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Kwanza | Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza

Kila mwaka, maelfu ya wanafunzi nchini Tanzania hufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi. Baada ya mtihani huu, wanafunzi waliofaulu hupangiwa shule za sekondari za Serikali ili kuendelea na masomo yao.

Wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza nchini Tanzania huchaguliwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vinavyotolewa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Mfumo huu una lengo la kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa darasa la saba anapata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari. Katika makala hii, tutaangazia vigezo muhimu vinavyotumika katika uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza.

Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza

Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza

Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na shule za bweni unazingatia vigezo vifuatavyo:

1. Ufaulu wa Mtahiniwa Katika Mtihani wa Darasa la Saba

Kigezo kikuu cha kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni ufaulu wa mwanafunzi katika mtihani wa darasa la saba.

Kila mwanafunzi anayefanya mtihani huu na kufikia alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300, anapata nafasi ya kujiunga na shule za sekondari za serikali. Mtahiniwa mwenye alama za chini ya kiwango hiki hawezi kuchaguliwa.

2. Vigezo vya Upendeleo Maalum

Zaidi ya ufaulu wa juu, vigezo vingine vya upendeleo vinaweza kuzingatiwa katika uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na shule za bweni za kidato cha Kwanza. Vigezo hivi ni pamoja na:

  • Maeneo ya Vijijini na Mazingira Magumu: Wanafunzi wanaotoka maeneo ya vijijini au yenye changamoto za kimaisha mara nyingi hupewa kipaumbele katika shule za bweni za kawaida. Hii inasaidia kuhakikisha usawa wa fursa za elimu kwa watoto wa maeneo haya.
  • Wanafunzi wa Kike: Kwa lengo la kuongeza usawa wa kijinsia katika elimu, kuna juhudi maalum za kuwapa nafasi zaidi wanafunzi wa kike kutoka maeneo ya vijijini au mazingira magumu kwenye shule za bweni.

Upangaji wa Shule za Sekondari

Shule za sekondari nchini zimegawanywa katika makundi makuu mawili: shule za kutwa na shule za bweni. Uchaguzi wa shule hizi unategemea nafasi zilizopo na ufaulu wa mwanafunzi.

a) Shule za Kutwa

Shule nyingi za sekondari nchini ni za kutwa, ambazo huchukua idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza. Wanafunzi wengi waliofaulu na kukidhi vigezo vya uchaguzi hupangiwa shule hizi kulingana na alama walizopata.

b) Shule za Bweni

Kwa upande wa shule za bweni, nafasi ni chache ikilinganishwa na shule za kutwa. Shule hizi zimegawanyika katika makundi matatu:

  • Shule za Wanafunzi Wenye Ufaulu wa Juu Zaidi almaharufu kama Shule za Vipaji Maalumu: Hizi ni shule maalum zinazochukua wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu kabisa.
  • Shule za Ufundi: Shule hizi zinachukua wanafunzi wenye vipaji vya kitaaluma na mwelekeo wa masomo ya ufundi.
  • Shule za Bweni Kawaida: Hizi ni shule za bweni zinazopokea wanafunzi wa kawaida kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, hasa kutoka vijijini au maeneo yenye mazingira magumu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Sababu Zinazofanya Wanafunzi Kufeli Mitihani ya NECTA
  2. Tarehe za Kujiandikisha Mitihani ya Taifa ya NECTA
  3. Mbinu za Kufaulu Mtihani wa wa NECTA Kidato cha Nne
  4. Orodha Kamili ya Masomo ya Mitihani ya NECTA Kidato cha Nne
  5. Orodha ya Masomo Shule ya Msingi
  6. Jinsi ya Kujiandaa na Mtihani wa NECTA- Mwongozo Kamili
  7. TCU Yatangaza Dirisha la Tatu la Udahili Vyuo Vikuu 2024/2025