Hatma ya Maxi Nzengeli Yanga, Mkopo Mpya au Ofa Maniema | MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Maxi Mpia Nzengeli, bado ni mchezaji halali wa AS Maniema Union, licha ya msimu huu kuwa kwa mkopo Yanga SC. Taarifa rasmi zinasema kuwa mkataba wake wa mkopo na Yanga unamalizika mwishoni mwa mwaka huu, na hatima yake bado haijafahamika.
Hatma ya Maxi Nzengeli Yanga, Mkopo Mpya au Ofa Maniema
Habari za uhakika zinasema tayari Yanga SC imeonyesha nia ya dhati ya kutaka kuinasa saini ya kudumu Nzengeli. Imeripotiwa kuwa mabingwa hao wa Tanzania walitoa ofa ya dola 200,000 kwa AS Maniema ili kumsajili moja kwa moja, lakini hadi sasa rais wa klabu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hajajibu rasmi ofa hiyo.

Katika hatua mpya, Yanga SC imepanga kuomba mkopo mwingine wa muda mrefu, safari hii kwa miaka miwili, ili kuendelea kupata huduma ya kiungo huyo mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi mbalimbali za ushambuliaji.
Hata hivyo, AS Maniema imeahirisha uamuzi wake wa mwisho ikisubiri ofa bora kutoka kwa vilabu vingine pia vinavyotaka kumsajili Nzengeli. Miongoni mwa klabu zinazoripotiwa kumfuatilia kwa karibu ni zile za Afrika Kusini na Morocco, nchi zenye soko kubwa la wachezaji wa Afrika ya Kati.
Kuhusu mchezaji huyo, habari zilizo karibu na klabu hiyo zinaeleza kuwa Nzengeli yuko tayari kubaki Yanga au kusaini klabu nyingine kulingana na uamuzi wa Maniema na hali ya mazungumzo baina ya wahusika.
CHECK ALSO:
- Raundi ya 29 NBC Ligi Kuu, Mechi Zote Nane Kupigwa Saa 10:00 Jioni Juni 18
- Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025
- Orodha ya Vilabu Bora Afrika CAF 2025 Club Ranking
- Viwango vya Ubora Barani Africa CAF Club Ranking 2025
- Ratiba ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Kariakoo Derby Yanga vs Simba Kuchezwa Juni 25, 2025
Weka maoni yako