Vitu vya Kuambatanisha Wakati wa Kuomba Mkopo HESLB 2025/2026 | Jinsi ya Kuomba Mkopo kwa Wanafunzi HELSB 2025/2026. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), itatangaza hivi karibuni ‘Mwongozo wa Utoaji Mkopo na Ruzuku kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026’ utakaopatikana katika www.heslb.go.tz kuanzia Julai 7, 2025.
Waombaji mkopo watarajiwa wanashauriwa kuusoma na kuuelewa mwongozo huo kabla ya kujaza fomu za maombi ya mikopo kupitia http://olas.heslb.go.tz ili kumwezesha mwombaji kujaza fomu kwa usahihi na ukamilifu/Vitu vya Kuambatanisha Wakati wa Kuomba Mkopo HESLB 2025/2026.
Vitu vya Kuambatanisha Wakati wa Kuomba Mkopo HESLB 2025/2026
(i) Cheti cha Kuzaliwa:
Cheti kinachotambuliwa rasmi na Mamlaka ya Serikali ya Mtaa au Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa waombaji waliozaliwa Tanzania Bara, au
Cheti kutoka Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) kwa waombaji kutoka Zanzibar.

(ii) Cheti cha Kifo cha Mzazi au Mlezi (ikiwa mwombaji ni yatima):
Kiwe ni cheti halali kilichotolewa na mamlaka zinazotambulika kama RITA au ZCSRA, kwa Tanzania Bara na Zanzibar mtawalia.
(iii) Barua ya Uthibitisho wa Uhitaji wa Msaada (Statement of Need):
Iwe imethibitishwa na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka wilaya au mkoa husika.
(iv) Fomu ya Taarifa za Mzazi/Mlezi (Parent/Guardian Form):
Ijazwe kikamilifu, sahihi na ithibitishwe na Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji anakoishi mzazi/mlezi wa mwombaji.
(v) Fomu ya Ufadhili wa Elimu kutoka kwa Mfadhili (Scholarship or Sponsorship Form):
Ikiwa mwombaji anapata ufadhili kutoka taasisi au shirika, fomu hiyo iwe na maelezo ya kina kuhusu ufadhili unaotolewa.
(vi) Nambari ya Utambuzi kutoka kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF ID):
Kwa waombaji wanaotoka katika kaya maskini zinazonufaika na mpango wa TASAF.
(vii) Uthibitisho wa Hali Ngumu ya Maisha kutoka kwa Ofisa Maendeleo ya Jamii:
Barua hii ni kwa ajili ya kuthibitisha hali ya maisha ya mzazi au mlezi, ikiwa ni pamoja na kuwa na ugonjwa sugu au kutokuwa na kipato cha kuweza kumhudumia mwombaji.
(viii) Barua ya Kifo cha Mzazi au Mlezi kutoka kwa Mamlaka za Serikali ya Mtaa:
Ikiwa mwombaji ni yatima au amepoteza mlezi wake, barua hii ni ya kuthibitisha tukio hilo kwa ajili ya maombi ya mkopo.
Waombaji wote wanapaswa kuhakikisha kuwa nyaraka zao ni sahihi, halali na zimeidhinishwa na mamlaka husika. Uwasilishaji wa taarifa za uongo unaweza kusababisha maombi kukataliwa au hatua za kisheria kuchukuliwa/Vitu vya Kuambatanisha Wakati wa Kuomba Mkopo HESLB 2025/2026.
CHECK ALSO:
- Jinsi ya Kuomba Mkopo kwa Wanafunzi HELSB 2025/2026
- TAMISEMI Second Selection Form Five 2025/2026
- Majina Waliochaguliwa Selection Form Five 2025 To 2026 Kidato cha Tano
- Majina Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano Form five Selection 2025
- Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Tano, 2025 TAMISEMI Form Five Selection
Weka maoni yako