KIKOSI cha Simba Leo vs KenGold 18/06/025 | Mechi Muhimu Katika Mbio za Ubingwa NBC Premier League. Simba SC kumenyana na Kengold FC Juni 18: Mechi muhimu kwa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
Simba SC itamenyana na Kengold FC Juni 18, 2025, saa 1:00 Usiku UTC, katika Ligi Kuu ya NBC 2024/2025. Mechi hii inachukuliwa kuwa muhimu sana kwa Simba SC kutokana na nafasi yao kwenye mbio za ubingwa.
Simba SC kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo, ikipigania taji hilo dhidi ya wapinzani wao wakuu. Hii ni fursa kwa klabu kuimarisha nafasi yake na kuweka presha kwa timu za juu. Matokeo mabaya katika mechi hii yanaweza kuathiri moja kwa moja nafasi ya Simba SC kutwaa ubingwa hivyo kuongeza presha kwa wakufunzi na wachezaji.
Kwa upande mwingine, Kengold FC tayari imeshuka daraja rasmi, ikishika nafasi ya 16 kwenye msimamo. Hii inafanya mechi hii kuwa ya heshima kwao, kwani matokeo yoyote watakayopata hayatabadilisha msimamo wao katika msimamo wa mwisho wa ligi. Hata hivyo, timu zinazokaribia kushuka daraja huwa zinacheza kwa uhuru na bila presha jambo ambalo linaweza kuwa changamoto kwa Simba SC wasipokuwa makini.
KIKOSI cha Simba Leo vs KenGold 18/06/025
Kikosi cha Simba kinachoaza leo dhidi ya Kengold kwenye mchezo wa NBC ligi kuu Tanzania bara kama kifuatacho:-

- CAMARA
- HUSEIN
- KAPOMBE
- CHAMOU
- CHEMALON
- KAGOMA
- MAVAMBO
- ATEBA
- AHOUA
- MPANZU
- KIBU
CHECK ALSO:
Weka maoni yako