Je Kariakoo Derby Kuamua Bingwa NBC Ligi Kuu 2024/2025? — Yanga vs Simba Juni 25. Yanga SC watakuwa wenyeji wa Simba SC Juni 25 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Derby.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki wanasubiri kwa hamu mchezo wa Kariakoo kati ya Young Africans (Yanga SC) dhidi ya Simba SC, utakaochezwa Jumatano ijayo, Juni 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba rasmi ya Bodi ya Ligi, mechi hiyo itaanza saa 11:00 Jioni na kurushwa moja kwa moja na Azam Sports 1 HD.
Je Kariakoo Derby Kuamua Bingwa NBC Ligi Kuu 2024/2025?
Derby hii haitakuwa ya kawaida; ni zaidi ya mashindano ya jadi ya kienyeji. Mechi hii ya raundi ya mwisho itakuwa ya kipekee, kwani mshindi atatangazwa kuwa bingwa rasmi wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/2025.

Yanga SC na Simba SC kwa sasa wanaongoza kwenye msimamo wakiwa na tofauti finyu ya pointi na mabao, jambo ambalo linaongeza ukali wa mechi. Matokeo ya mechi hii yatakuwa na umuhimu wa kihistoria kwa mashabiki, waamuzi na wachezaji wa vilabu vyote viwili.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi tayari wametekeleza hatua za kiusalama ili kuhakikisha mechi hiyo inakwenda vizuri na mashabiki wafurahie tukio hilo salama. Tikiti zinatarajiwa kuuzwa mtandaoni na kwa idadi ndogo kutokana na hatua za usalama.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako