Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025

Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025 | Fursa Mpya za Watumishi wa Afya Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeendelea na jitihada za kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania kwa kuajiri wataalamu wapya katika sekta hiyo muhimu.

Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025

Katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, wito wa Kuajiri Watumishi wa Afya 2025 ulizinduliwa rasmi, ukiwalenga wataalamu kutoka sekta mbalimbali za afya wanaoomba kuajiriwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati kote nchini.

Lengo la ajira hizo ni kuongeza nguvu kazi ya kitaaluma ili kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa vijijini na maeneo ya pembezoni ambayo bado yanakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa afya.

Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025
Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025

Maelezo Muhimu Kuhusu Nafasi za Ajira za Afya 2025

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, nafasi hizi zitajumuisha kada mbalimbali zikiwemo:

  • Madaktari Bingwa na Madaktari wa kawaida

  • Wauguzi (Ngazi ya Shahada, Stashahada na Cheti)

  • Wafamasia

  • Wataalamu wa Maabara ya Afya

  • Wataalamu wa Mionzi

  • Wataalamu wa Lishe

  • Wataalamu wa Afya ya Jamii

  • Wateknolojia wa Dawa na Vifaa Tiba

  • Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHWs)

Ajira hizi ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya, bila kujali mahali alipo/Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025.

Vigezo na Masharti kwa Waombaji

Waombaji wa nafasi hizi wanapaswa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

  1. Kuwa Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.

  2. Kuwa na vyeti halali vya taaluma kutoka chuo kinachotambulika na Baraza husika.

  3. Kuwa na usajili wa kitaaluma kutoka bodi au baraza husika (mfano, Baraza la Madaktari, Baraza la Wauguzi n.k.)

  4. Kuwa na cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

  5. Kuwa tayari kufanya kazi katika maeneo yoyote yatakayopangwa na Serikali, hasa katika vituo vya afya vilivyopo pembezoni.

Wizara ya Afya imetangaza kuwa maombi yote yatawasilishwa kupitia tovuti rasmi ya manunuzi ya serikali, ambapo waombaji wanapaswa kujisajili, kukamilisha taarifa zao na kupakia nakala za vyeti vinavyohitajika/Tangazo la Nafasi za Kazi Ajira za Afya 2025.

Tarehe rasmi ya ufunguzi wa maombi, pamoja na tarehe ya mwisho ya kutuma maombi, imeelezwa kwa kina katika tangazo kamili lililochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).

CHECK ALSO:

  1. Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
  2. Hili Hapa Tangazo la Nafasi za Kazi LGAs June 2025
  3. MDAs & LGAs Nafasi za Ajira Mpya 8894, Juni 2025
  4. Tangazo la Nafasi 2326 za Kazi Serikalini Tanzania Juni 2025 MDAs, LGAs na Wizara ya Ardhi