Tanzania Miongoni mwa Nchi 12 Zitakazoingiza Timu 4 CAF 2025/26 | CAF yatangaza nchi 12 ambazo zimeshinda nafasi ya kuingia timu nne katika mashindano ya 2025/26 | Tanzania pamoja
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) kupitia TFF, limetangaza rasmi orodha ya nchi 12 zilizoshinda nafasi ya kuingia jumla ya timu nne katika mashindano ya kimataifa ya vilabu ya CAF 2025/2026: Ligi ya Mabingwa CAF na Kombe la Shirikisho la CAF.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashindano hayo yataanza rasmi kwa hatua ya awali kati ya Septemba 19 na 21, 2025, na Septemba 26 na 28, 2025.
Tanzania Miongoni mwa Nchi 12 Zitakazoingiza Timu 4 CAF 2025/26
Nchi 12 Zilizopata Nafasi ya Kuingiza Timu 4 Katika CAF 2025/26(Tanzania Miongoni mwa Nchi 12 Zitakazoingiza Timu 4 CAF 2025/26):
Tanzania ๐น๐ฟ
Algeria ๐ฉ๐ฟ
Angola ๐ฆ๐ด
Ivory Coast (Cรดte d’Ivoire) ๐จ๐ฎ
Misri ๐ช๐ฌ
Libya ๐ฑ๐พ
Morocco ๐ฒ๐ฆ
Nigeria ๐ณ๐ฌ
DR Congo ๐จ๐ฉ
Afrika Kusini ๐ฟ๐ฆ
Sudan ๐ธ๐ฉ
Tunisia ๐น๐ณ
Hii ni ishara ya kuimarika kwa viwango vya soka katika mataifa haya, ambapo kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayofanya vizuri hasa kutokana na mafanikio ya klabu za Yanga SC, Simba SC, Namungo FC na timu nyingine zinazoshiriki mashindano ya CAF.
Kupata nafasi ya kusajili timu nne ni heshima kubwa na fursa ya kukuza mashindano ya ndani, kuongeza thamani ya ligi, na kuwapa wachezaji wa ndani nafasi ya kuonyesha vipaji vyao Afrika.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako