TETESI za Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Wanaoitajika 2025/2026 | Raouf Memel Dao Ajiunga Rasmi na Singida BS Kutoka AS Sonabel. Raouf Memel Dao amejiunga na Singida BS kutoka Burkina Faso kwa mkataba wa miaka mitatu.
TETESI za Usajili Singida Black Stars, Wachezaji Wanaoitajika 2025/2026
Klabu ya Singida Big Stars ya Tanzania (Singida BS) imefanikiwa kumsajili Raouf Memel Dao mwenye umri wa miaka 21, mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Burkina Faso msimu uliopita. Kiungo mshambuliaji anajiunga na Singida BS kutoka AS Sonabel ya Burkina Faso.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Dao amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Ujio wake unaonekana kuwa hatua muhimu katika kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Singida BS kuelekea msimu mpya wa ligi.

Dao, ambaye alitunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora (MVP) wa Ligi Kuu ya Burkina Faso, anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi, kasi yake na uwezo wake wa kufunga mabao muhimu. Ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, akichangia kwa kiasi kikubwa kwenye mashambulizi na kuunganisha safu ya kiungo na washambuliaji.
Kusainiwa kwa Dao kunaonyesha dhamira ya Singida BS katika kufanya mabadiliko ya kisasa na kushindana vikali zaidi katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hii ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuingiza vipaji vya kigeni ili kuongeza ushindani na ubora wa kikosi chake.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako