TETESI ZA USAJILI YANGA, Ibrahima Keita Kujiunga na Yanga SC, Mazungumzo Yafikia Hatua Nzuri. Ibrahima Keita anaondoka TP Mazembe, na Yanga SC yaweka kipaumbele usajili wake.
Ibrahima Keita Kujiunga na Yanga SC, Mazungumzo Yafikia Hatua Nzuri
Beki wa kulia wa Mauritania Ibrahima Keita, 23, ameondoka rasmi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), licha ya kuwa na mkataba hadi Juni 30, 2025.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Keita hatashiriki mechi yoyote ya TP Mazembe iliyosalia msimu huu. Uamuzi huu unaonyesha kuwa mchezaji huyo amefungua maisha mapya ya soka nje ya DRC.
Hadi sasa mazungumzo kati ya Keita na klabu ya Yanga SC ya Tanzania yapo katika hatua nzuri, na pande zote mbili zinaonekana kutaka kufikia muafaka haraka iwezekanavyo. Uamuzi wa mwisho sasa ni wa Yanga SC kukamilisha mchakato wa uhamisho.
Keita ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa katika nafasi ya beki wa kulia. Anajulikana kwa kasi yake, uwezo wa kuzuia, na pasi za mabao, na hivyo kumfanya kuwa chaguo la kuvutia kwa timu inayotaka kuimarisha safu yake ya ulinzi.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako