Kagera Sugar na KenGold Wasuka Daraja, Playoff ni Fountain Gate na Tanzania Prisons

Kagera Sugar na KenGold Wasuka Daraja, Playoff ni Fountain Gate na Tanzania Prisons | Matokeo ya Mechi za Mwisho Ligi Kuu Tanzania 2024/2025.

Msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2024/2025 NBC umekamilika rasmi leo Juni 22, 2025 kwa mechi kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti nchini. Hata hivyo, pazia hilo litafungwa rasmi Juni 25 kwa fainali kati ya mahasimu wa jadi Simba SC na Yanga SC, itakayoamua bingwa wa ligi hiyo na kukamilisha msimu wa mechi 30.

Kagera Sugar na KenGold Wasuka Daraja, Playoff ni Fountain Gate na Tanzania Prisons

  • Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji FC
    Mabao: Chama (04’), Duke (50’), Bacca (62’), Onyango (90’+4), Maxi (90’+7)

  • Simba SC 1-0 Kagera Sugar
    Bao: Mukwala (17’)

  • Fountain Gate 2-3 Azam FC
    Mabao: Mokono (45’p) / Zidane (03’), Shiga (23’ OG), Sopu (90’+2p)

  • Namungo FC 5-0 KenGold FC
    Mabao: Kagere (07’, 29’), Kabunda (41’), Nyoni (45’), Karabaka (90’+1)

  • Singida Black Stars 3-3 Tanzania Prisons
    Mabao: Pokou (43’), Tchakei (45’+), Sowah (47’) / Ismail (63’p, 76’p), Musa (84’)

  • Pamba Jiji 1-1 KMC FC
    Mabao: Mathew Tegis (34’) / —

  • Coastal Union 1-1 Tabora United
    Mabao: Kikoti (90’p) / Mwanunongo (53’)

  • Mashujaa FC 0-0 JKT Tanzania
    Hakukuwa na mabao.

Kagera Sugar na KenGold Wasuka Daraja, Playoff ni Fountain Gate na Tanzania Prisons
Kagera Sugar na KenGold Wasuka Daraja, Playoff ni Fountain Gate na Tanzania Prisons

Kwa ujumla, michezo ya leo imeshuhudia jumla ya mabao 26 yakifungwa, huku timu ya Lake Tanganyika FC kutoka Kigoma pekee ikiwa haikushiriki siku ya leo.

Hatma ya Msimu 2024/25:

  • Zimeshuka Daraja:

    • Kagera Sugar FC

    • KenGold FC

Timu hizi zimeshindwa kujinasua kutoka nafasi mbili za mwisho na hivyo kushuka rasmi daraja.

  • Mtoano (Playoff):

    • Fountain Gate FC

    • Tanzania Prisons FC

Timu hizi zitashiriki hatua ya mtoano dhidi ya timu kutoka Championship kwa ajili ya kuwania nafasi ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Mchezo wa mwisho wa msimu huu utakuwa ni Simba SC dhidi ya Yanga SC, utakaopigwa Juni 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Hii haitakuwa mechi yoyote tu, bali ndiyo itakayoamua bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/2025, huku timu zote zikiwania ubingwa.

Katika msimu wa 2024/2025 mashabiki wa soka nchini wameshuhudia ushindani mkubwa, mabao mengi na matokeo ya kustaajabisha. Mashabiki wanashauriwa kufuatilia kwa karibu mchezo wa fainali baina ya timu zao za nyumbani, kwani ndio utakaoamua mshindi wa ligi hiyo, jambo ambalo ni nadra kutokea katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa ratiba ya mchujo au taarifa kuhusu tarehe ya mwisho ya usajili, tafadhali tembelea tovuti yetu kwa taarifa sahihi na zilizosasishwa.

CHECK ALSO:

  1. Yanga SC vs Dodoma Jiji Leo Saa Ngapi 22/06/2025
  2. KIKOSI Cha Yanga SC Leo vs Dodoma Jiji 22/06/2025
  3. Matokeo ya Yanga SC Leo vs Dodoma Jiji 22/06/2025
  4. Simba SC vs Kagera Sugar Leo Sangapi 22/06/2025