Yanga SC vs Simba SC, Derby Kuamua Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2024/25 | Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 utaamuliwa katika mechi ya mwisho ya msimu huu, Kariakoo derby, kati ya vigogo wa soka nchini, Yanga SC na Simba SC. Pambano hili la kihistoria litachezwa Jumatano, Juni 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Yanga SC vs Simba SC, Derby Kuamua Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2024/25
Jedwali baada ya Siku ya Mechi 30:
- Yanga SC inaongoza msimamo ikiwa na pointi 79 baada ya mechi 29.
- Simba SC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 78, pia baada ya mechi 29.
Kulingana na matokeo haya, mechi ya mwisho kati ya timu hizi mbili itaamua bingwa wa msimu huu. Yanga SC inahitaji sare au ushindi ili kutwaa ubingwa, wakati Simba SC lazima ishinde mechi ili kuwapita kwa pointi na kutwaa ubingwa.

Matokeo ya Timu zote Raundi ya 30:
FT: Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji FC
Mabao:
⚽ 03’ – Clatous Chama
âš½ 52’ – Stephane Aziz Ki “Duke”
⚽ 62’ – Stephane Bacca
⚽ 90+2’ – Kennedy Onyango
⚽ 90+5’ – Maxi NzengeliFT: Simba SC 1-0 Kagera Sugar
Bao pekee la mchezo:
⚽ 17’ – Steven Mukwala
Kwa msimu wa 2024/25, ushindani kati ya Simba na Yanga umefikia kilele. Ligi hiyo imekuwa na ushindani mkali, na sasa mashabiki wote wanaitazama Kariakoo derby Juni 25 kuamua nani atawazwa bingwa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako