Viingilio Mechi ya Yanga vs Simba 25 Juni 2025 | Yanga SC imetangaza rasmi ratiba ya kukata tiketi ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya wapinzani wa jadi Simba SC.
Mechi hii muhimu itachezwa Jumatano, Juni 25, 2025, saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Viingilio Mechi ya Yanga vs Simba 25 Juni 2025

Mzunguko: TSh 5,000
Orange: TSh 10,000
VIP C: TSh 20,000
VIP B: TSh 30,000
VIP A: TSh 50,000 (Zote ZIMEISHA)
Kwa mujibu wa tangazo hilo, tiketi za VIP A, kitengo cha juu zaidi, tayari zimeuzwa, kuonyesha ukubwa na mvuto wa mchezo huu maarufu wa Kariakoo derby.
Mashabiki wote wanaombwa kununua tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi, hasa kutokana na wingi wa watu wanaotarajiwa uwanjani.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako