Azam Yathibitisha Kuachana na Gibril Sillah | Azam FC imethibitisha kuachana rasmi na winga wake kutoka Gambia, Gibril Sillah, baada ya kumalizika rasmi kwa mkataba wake.
Azam Yathibitisha Kuachana na Gibril Sillah
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Chamazi, Sillah, 26, anaondoka baada ya miaka kadhaa ya mafanikio akiwa na timu hiyo.
Gibril Sillah ameichezea Azam FC jumla ya mechi 68. Kwa muda huo, amefunga mabao 21 na kutoa pasi za mabao 10, akionyesha uwezo wake wa hali ya juu katika safu ya ushambuliaji ya Wanalambalamba.

Kwa wakati huu, haijajulikana ni klabu gani itamsajili mchezaji huyo, huku mashabiki na wapenzi wa soka wakifuatilia kwa karibu maendeleo yake.
Azam FC kupitia tovuti yake rasmi, imemshukuru Sillah kwa mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo na kumtakia kila la kheri katika hatua inayofuata ya maisha yake ya soka.
CHECK ALSO:
shida ya sillah hakabi