Fabrice Ngoma Aaga Simba Rasmi Baada ya Miaka Miwili | Kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Luamba Ngoma (31) ametangaza rasmi kuachana na klabu ya Simba Sports Club baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili. Ngoma alijiunga na klabu hiyo Julai 14, 2023, akitokea klabu ya Al-Hilal ya Sudan.
Ngoma alithibitisha kuondoka kwake kupitia ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa kijamii Juni 29, 2025, akitoa shukurani zake kwa bodi ya wakurugenzi, makocha, wachezaji wenzake na mashabiki wa Simba SC.
Fabrice Ngoma Aaga Simba Rasmi Baada ya Miaka Miwili
Katika ujumbe wake wa kuaga, Ngoma alisema:
“Nataka kuchukua wasaa huu kuwashukuru kila mmoja aliyefanya nijisikie nyumbani hapa Simba SC… Hatukufikia baadhi ya malengo yetu lakini kumbukumbu zote zitasalia akilini na moyoni mwangu milele.”
Ngoma pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Kocha Fadlu Davids kwa kazi nzuri na kuwataka mashabiki kuendelea kuiunga mkono klabu hiyo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako