Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily SC ya Misri | Aliyekuwa meneja wa Yanga SC Miloud Hamdi amejiunga rasmi na Ismaily SC ya Ligi Kuu ya Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily SC ya Misri
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyo karibu na klabu hiyo, Hamdi amekubali mkataba wa kuvutia utakaomwezesha kuongeza mara mbili ya mshahara wake kama meneja wa Yanga SC ya Tanzania. Hii ni hatua muhimu kwa meneja huyo ambaye ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika.
Ismaily SC inatarajiwa kumtangaza rasmi meneja Miloud Hamdi leo, na maandalizi ya uwasilishaji rasmi tayari yameanza nchini Misri.

Meneja Miloud Hamdi aliiongoza Yanga SC kwa mafanikio kadhaa kabla ya kuondoka, na sasa anatarajia kukuza ujuzi wake wa kiufundi katika soka la Afrika Kaskazini.
Hatua hii inadhihirisha kuwa makocha wanaofanya vizuri katika soka la Afrika Mashariki wanaweza kupata kazi katika klabu kubwa za Afrika Kaskazini zenye mifuko mirefu.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako