Himid Mao Mkami Karibu Kujiunga Tena na Azam, Baada ya Kumaliza Mkataba na Tala’ea El Gaish. KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami anaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho ya kurejea Azam FC, baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Tala’ea El Gaish ya Ligi Kuu ya Misri.
Mao ambaye alicheza vyema Azam FC kabla ya kutimkia kimataifa, anatarajiwa kujiunga na timu hiyo ya Dar es Salaam iwapo makubaliano ya mwisho yatafikiwa. Usajili huo ukikamilika utaimarisha kwa kiasi kikubwa safu ya kiungo ya Azam FC kuelekea msimu ujao wa mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Iwapo atasajiliwa, Himid Mao atakuwa miongoni mwa wachezaji wapya waliothibitishwa kuichezea Azam FC msimu huu, akiwemo kipa mahiri Aishi Manula, pamoja na chipukizi Muhsini Malima na Lameck Lawi. Hii inadhihirisha kuwa Azam FC imejipanga vyema kwa ajili ya msimu wa 2025/2026, huku ikiboresha kikosi mapema.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako