Singida Black Stars Yamtambulisha Gamondi Kuwa Kocha Mkuu: Klabu ya Singida Black Stars imemteua rasmi kocha mkuu wa zamani wa Young Africans SC Miguel Ángel Gamondi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Uteuzi huu umetangazwa leo Julai 3, 2025 kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo.
Singida Black Stars Yamtambulisha Gamondi Kuwa Kocha Mkuu
Gamondi raia wa Argentina amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa nia ya kuinoa klabu ya Singida Black Stars kwenye msimu mpya wa ligi kuu ya NBC na mashindano mengine msimu wa 2025/2026.
Mabadiliko haya yanafanya wafanyikazi wa klabu hiyo kuimarishwa, huku aliyekuwa kocha mkuu David Ouma na Moussa N’Daw wakihudumu kama makocha wasaidizi wa Gamondi. Mabadiliko haya yameidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu kwa ajili ya msimu ujao.

“Wakati huo huo, mabadiliko haya katika benchi la ufundi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Gamondi ni kocha mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika, na amewahi kufundisha vilabu mbalimbali pamoja na kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa. Uongozi wa Singida Black Stars una matumaini makubwa kuwa ujio wake utaongeza ufanisi, nidhamu, na ushindani ndani ya kikosi.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako