Yanga Yatoa Msimamo wa Aziz Ki na Kufichua Ujio wa Kocha Mpya | Yanga SC yaweka wazi mustakabali wa Stéphane Aziz Ki na kumthibitisha kocha wake mpya
BODI ya Young Africans SC (Yanga) imeweka wazi msimamo wake kuhusu mustakabali wa kiungo nyota Stéphane Aziz Ki, ambaye yuko kwa mkopo wa muda mfupi katika klabu ya Wydad AC ya Morocco.
Yanga Yatoa Msimamo wa Aziz Ki na Kufichua Ujio wa Kocha Mpya
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amefafanua kuwa:
“Bado ana mwaka mmoja na klabu yetu. Makubaliano yetu na Wydad yalihusu mkataba wa miezi mitatu tu.”
Kamwe aliongeza kuwa iwapo Wydad haitamhitaji kiungo huyo kwa mkataba wa kudumu, Aziz Ki atarejea Tanzania kucheza mechi ya Ngao ya Jamii, itakayoanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ujio wa kocha mpya umethibitishwa
Aidha, Kamwe alithibitisha kuwa kocha mpya wa Yanga amewasili nchini na anapitia taarifa na historia ya kikosi cha awali cha makocha kabla ya kuwasilishwa rasmi.
“Kocha wetu mpya anaifahamu vizuri Yanga,” amesema Kamwe, akionyesha matumaini makubwa kwa msimu ujao.
Kwa sasa, mashabiki wa Yanga wanatarajia kutambulishwa kwa kocha huyo, ambaye kwa mujibu wa Kamwe, anaelewa vema mazingira ya timu hiyo kongwe yenye mafanikio lukuki barani Afrika Mashariki.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako