Fountain Gate Yasalia Ligi Kuu NBC 2025/26, Ushindi Dhidi ya Stand United

Fountain Gate Yasalia Ligi Kuu NBC 2025/26, Ushindi Dhidi ya Stand United: Fountain Gate FC imebakia na nafasi yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2025/26 baada ya kuifunga Stand United.

Fountain Gate FC imefanikiwa kusalia Ligi Kuu ya Tanzania Bara NBC kwa msimu wa 2025/26 baada ya kuifunga Stand United kwa jumla ya mabao 5-1 katika mechi ya mtoano.

Katika mechi ya marudiano ya hivi majuzi, Fountain Gate alionyesha uwezo mkubwa kwa kupata ushindi wa mabao 2-0, na kukamilisha ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya kushinda pia mechi ya awali 3-1.

Fountain Gate Yasalia Ligi Kuu NBC 2025/26, Ushindi Dhidi ya Stand United

Mabao ya Fountain Gate kwenye mchezo wa pili yalifungwa na:

Fountain Gate Yasalia Ligi Kuu NBC 2025/26, Ushindi Dhidi ya Stand United

  • âš½ Ellie Mokono dakika ya 51

  • âš½ William Edgar kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90+1

Kwa matokeo haya, Stand United wameshindwa kurejea Ligi Kuu na hivyo kusalia Ligi ya Championship kwa msimu ujao, wakati Fountain Gate wakijihakikishia kushiriki tena kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara.

CHECK ALSO:

  1. Yanga Kushiriki Champions Tournament Nchini Namibia Agosti 2025
  2. Kennedy Musonda Ajiunga na Hapoel Ramat Gan ya Israel
  3. Ratiba Kamili ya LaLiga 2025/2026
  4. Ratiba El Clasico 2025/2026, Real Madrid vs Barcelona Oktoba 26 na Mei 10