Lassine Kouma Kutua Yanga, Simba SC Wajiondoa: Katika habari za hivi punde kutoka soko la kimataifa la usajili, klabu ya Simba Sports Club imethibitisha kujitoa katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Mali Lassine Kouma mwenye umri wa miaka 21. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya klabu hiyo, hakutakuwa na majadiliano zaidi kati ya Simba na mchezaji huyo.
Lassine Kouma Kutua Yanga, Simba SC Wajiondoa
Uamuzi huo umekuja wakati mahasimu wao, Young Africans SC (Yanga), wakikaribia kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wa kizazi kipya mwenye kipaji na uwezo mkubwa.
Lassine Kouma ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza kama mchezeshaji wa kati (central midfielder) na kiungo wa ushambuliaji. Ana asili ya taifa la Mali 🇲🇱 na ameonyesha kiwango bora katika michuano ya vijana na ligi kuu nchini kwake.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, ameonyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho (key passes), kusoma mchezo, na kuhimili presha katika maeneo ya kati—sifa ambazo zimekuwa kivutio kwa klabu mbalimbali ndani ya Afrika Mashariki.

Sababu za Simba SC Kujiondoa
Ingawa taarifa rasmi kutoka Simba SC hazijawekwa wazi hadharani, wachambuzi wa soka wanaamini sababu za Simba kujiondoa zinaweza kuwa ni:
-
Kutoafikiana katika masuala ya kimkataba au ada ya uhamisho.
-
Mabadiliko ya kipaumbele cha benchi la ufundi.
-
Ushindani wa moja kwa moja kutoka kwa Yanga SC, ambao walionyesha nia ya dhati na haraka katika kufanikisha uhamisho huu.
Kwa upande wa Yanga SC, taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji zinaonyesha kuwa mazungumzo yako katika hatua za mwisho. Endapo dili litakamilika, Lassine Kouma anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano mbalimbali na klabu ya Yanga kwa msimu wa mashindano wa 2025/20256.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako