Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria

Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria: Abdulhamid Moalin aondoka Yanga SC baada ya mkataba kumalizika | Sead Ramovic anajiunga na CR Belouizdad

Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria

Abdulhamid Moalin, mkurugenzi wa zamani wa ufundi na kocha msaidizi wa Young Africans SC (Yanga), hatakuwa sehemu ya makocha wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026. Hii inafuatia kumalizika kwa mkataba wake na makubaliano kati ya pande zote mbili kusitisha ushirikiano wao.

Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria

Moalin aliyejiunga na Yanga akitokea KMC katikati ya msimu uliopita, amethibitisha kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba. Bodi ya Yanga imeeleza kuridhia maamuzi hayo hasa baada ya kocha mpya Romain Folz kudai kuwa na kikosi chake cha makocha ambacho kilifungua njia kwa mabadiliko hayo.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na klabu hiyo zinasema kuwa Abdulhamid Moalin pamoja na aliyekuwa mchambuzi wa video wa Yanga wanapanga kuungana na Sead Ramovic ambaye msimu uliopita alikuwa kocha mkuu wa Yanga SC na sasa amejiunga na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria.

Hivi karibuni Yanga SC itamtambulisha Paul Matthews (53) kuwa Mkurugenzi wao mpya wa ufundi akichukua nafasi ya Moalin.

CHECK ALSO:

  1. Taifa Stars Yatoka Nyuma na Kuichapa Senegal 2-1, CECAFA Mataifa Matatu 2025
  2. Jezi Mpya za Simba SC 2025/2026
  3. Simba SC Wamuweka Mezani Privat Djéssan Bi wa Zoman FC
  4. Fei Toto Kujiunga na Simba kwa Mkataba wa Miaka Miwili