Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars

Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars: Simba SC imemsajili Jonathan Sowah kutoka Singida Black Stars kupitia makubaliano maalum.

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha rasmi kuwa mshambuliaji wake chaguo la kwanza Mghana Jonathan Sowah amejiunga na Simba SC kwa uhamisho wa kudumu. Utiaji saini huo ulifanywa kupitia makubaliano maalum kati ya pande zote mbili.

Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars

Taarifa rasmi iliyotolewa na Singida BS imesema:

“Uongozi wa Singida BS unawataarifu mashabiki, wapenzi na wadau wote wa soka kuwa umeridhia Simba SC kumsajili mchezaji wetu tegemeo Jonathan Sowah kwa uhamisho wa kudumu kwa MAKUBALIANO MAALUM.”

Taarifa hiyo pia ilibainisha kuwa makubaliano yalifikiwa kati ya Meneja wa Singida Black Stars, Rais wa heshima wa Simba SC, na uongozi wa klabu zote mbili, hatua inayoashiria ushirikiano wa karibu na wa kirafiki kati ya pande hizo.

Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars
Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars

“Tunamtakia Jonathan Sowah kila la heri katika changamoto mpya na tunamshukuru kwa kuitumikia vyema klabu yetu katika kipindi chote alichokuwa nasi.”

Jonathan Sowah ameonyesha uwezo mkubwa wa kushambulia akiwa na klabu ya Singida Black Stars kitu ambacho kimewavutia Simba SC wanaoendelea kujifua kwa msimu wa 2025/2026 na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

CHECK ALSO:

  1. Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria
  2. Taifa Stars Yatoka Nyuma na Kuichapa Senegal 2-1, CECAFA Mataifa Matatu 2025
  3. Jezi Mpya za Simba SC 2025/2026
  4. Simba SC Wamuweka Mezani Privat Djéssan Bi wa Zoman FC