Gharama za Kujisajili Mitihani ya NECTA
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) husimamia mitihani mbalimbali nchini, kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi elimu ya juu. Kwa wale wanaojiandaa kufanya mtihani wowote ule unaosimamiwa na NECTA, ni muhimu kuwa na uelewa wa kina kuhusu gharama za usajili ili kuhakikisha mchakato unaenda vizuri na kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.
Hapa tumekuletea muongozo kamili na wa kuhusu ada za usajili wa mitihani mbalimbali inayotolewa na NECTA. Taarifa hizi zitakusaidia kuelewa vyema gharama zinazohusika na kufanya maandalizi stahiki kabla ya kuanza mchakato wa usajili. Ni muhimu kutambua kuwa ada hizi zinaweza kubadilika, hivyo inashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) ili kupata taarifa zilizosasishwa.
Aina za Mitihani na Ada za Usajili wa Mitihani ya NECTA
Baraza lamitihani Tanzania NECTA husimamia mitihani mbalimbali kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi elimu ya juu. Ada za usajili hutofautiana kulingana na aina ya mtihani. Hapa chini kuna orodha ya mitihani na ada zake:
Aina ya Mtihani | Ada ya Usajili wa Kawaida | Ada ya Usajili wa Kuchelewa |
Cheti cha Elimu ya Msingi (kwa Kiingereza) | TZS 15,000 | N/A |
Mtihani wa Maarifa (QT) | TZS 30,000 | TZS 40,000 |
Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) | TZS 50,000 | TZS 65,000 |
Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari (ACSEE) | TZS 50,000 | TZS 65,000 |
Cheti cha Mwalimu Daraja A | TZS 50,000 | TZS 65,000 |
Stashahada ya Elimu ya Sekondari | TZS 50,000 | TZS 65,000 |
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka maoni yako