Simba Yaalikwa Kwenye Mchezo wa Kirafiki na JS Kabylie Agosti 18: JS Kabylie wa Algeria ameialika rasmi klabu ya Simba SC ya Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki nchini Algeria Agosti 18, 2025. Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya klabu hizo mbili kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Simba Yaalikwa Kwenye Mchezo wa Kirafiki na JS Kabylie Agosti 18
JS Kabylie, moja ya klabu maarufu na yenye mafanikio katika soka la Afrika Kaskazini, imeonyesha nia yake kubwa ya kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu na Simba SC.

Malengo ya Ushirikiano Huo:
📌 Kubadilishana uzoefu wa kiufundi na kitaasisi katika soka la kisasa
📌 Kuanzisha mechi za kirafiki za mara kwa mara baina ya vilabu hivyo
📌 Kukuza maendeleo ya vijana na benchi la ufundi kupitia warsha na mafunzo ya pamoja
📌 Kujenga ushirikiano wa kibiashara na kijamii kati ya vilabu hivyo viwili
Ushirikiano huu unaonekana kuwa fursa adhimu kwa Simba SC kuimarisha hadhi yake kimataifa, hasa kwa kushirikiana na klabu za Afrika Kaskazini zenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya CAF.
Kwa upande mwingine, JS Kabylie ananufaika na fursa ya kujiunga na klabu maarufu Afrika Mashariki iliyoshiriki kwa mafanikio mashindano ya kimataifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako