Simba SC Yasaini Mkataba wa Udhamini na Betway wa Bilioni 20 kwa Miaka Mitatu: Simba SC imepiga hatua kubwa katika biashara yake baada ya kutangaza rasmi mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri ya Betway, wenye thamani ya shilingi bilioni 20 (Sh20 bilioni) katika kipindi cha miaka mitatu.
Hii inamaanisha kuwa klabu hiyo itaingiza wastani wa shilingi bilioni 6.6 (Sh6 bilioni) kila mwaka, hatua inayodhihirisha dhamira ya klabu hiyo kufikia viwango vya juu zaidi barani Afrika.
Simba SC Yasaini Mkataba wa Udhamini na Betway wa Bilioni 20 kwa Miaka Mitatu
Wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa Simba SC, Zubeda Sakuru alieleza kuwa udhamini huu ni sehemu ya mkakati wa klabu kufanya kisasa na kuweka msingi wa mafanikio ya muda mrefu.

“Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,” alisema Bi. Sakuru.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania Bw.Jimmy Masaoe amewahakikishia mashabiki wa Simba SC kuwa watarajie huduma bora na za kisasa kutoka kwa mdhamini wao mpya. Alieleza kuwa Betway imejipanga kutoa huduma za hali ya juu, pamoja na ofa maalum kwa mashabiki wa Simba SC.
“Mashabiki wategemee huduma bora kutoka kwetu, tumejipanga. Lakini pia kutakuwa na huduma mbalimbali ambazo tumezibuni kwa ajili ya mashabiki wa Simba,” alisema Bw. Masaoe.
Betway, kama mojawapo ya kampuni zinazoongoza duniani za kamari za michezo, ina uwezo wa kudhibiti idadi kubwa ya wateja kwa wakati mmoja. Zaidi ya hayo, inatoa huduma kwa wateja 24/7, na kuongeza imani ya mtumiaji na usalama/Simba SC Yasaini Mkataba wa Udhamini na Betway wa Bilioni 20 kwa Miaka Mitatu.
Mkataba huu mpya kati ya Simba SC na Betway sio tu unaongeza thamani ya kibiashara ya klabu bali pia unaashiria enzi mpya ya ukuaji wa kitaasisi na kiteknolojia kwa Simba. Ni uamuzi ambao mashabiki wote wanapaswa kuuunga mkono, kwa lengo la kuifanya Simba kuwa klabu ya kimataifa kweli.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako