Mbeya City FC Yafanya Maboresho ya Kikosi, Yawaaga Wachezaji 9 na Kusajili 3: Klabu ya Mbeya City FC ikiwa ni miongoni mwa wachezaji wapya waliopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, inaendelea kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya ushindani mkali unaotarajiwa msimu ujao.
Mbeya City FC Yafanya Maboresho ya Kikosi, Yawaaga Wachezaji 9 na Kusajili 3
Kwa mujibu wa taarifa rasmi za klabu, wachezaji tisa (9) wameachiliwa, wachezaji wapya watatu (3) wamesajiliwa, na watatu (3) wameongezewa mikataba kutokana na mchango wao mzuri msimu uliopita.
Wachezaji Wapya Waliosajiliwa:
-
Omary Chibada
-
Ibrahim Ame
-
Kingu Pemba

Wachezaji Walioongezewa Mikataba:
-
Memory Pillar
-
Baraka Maranyingi
-
Eliud Ambikile
Wachezaji Walioachwa:
-
Kilaza Mazoea
-
Pius Joseph
-
Jeremiah Thomas
-
Fred Mlelwa
-
Mudathir Abdallah
-
Andrew Kihumbi
-
Feisal Mganga
-
Medson Mwakatundu
-
Chesco Mwasimba
Uongozi wa Mbeya City FC umeweka wazi kuwa maboresho haya ni sehemu ya maandalizi makini ya kuhakikisha klabu hiyo inaimarika na inabaki Ligi Kuu kwa muda mrefu, badala ya kurudi haraka Ligi Daraja la Kwanza.
Kuendelea kuimarika kwa Mbeya City FC kunaonyesha dhamira ya dhati ya klabu hiyo ya kuwa na kikosi imara chenye uwezo wa kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Mashabiki na wadau wa soka wanapaswa kufuatilia kwa karibu matukio haya na kutarajia zaidi kutoka kwa uongozi wa klabu katika siku zijazo.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako